Basi la abiria la Kampuni ya Kilimanjaro Express linalofanya safari zake Dar es salaam na Arusha limepata ajali eneo la Mkata, mkoani Tanga leo Jumapili Mei 5, 2019.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Tanga (RTO), Solomon Mwangamilo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kuwa basi hilo limepinduka.

“Ni kweli kuna basi la Kilimanjaro Express limeacha njia na kupinduka eneo la Mkata, kwa sasa ndio naelekea eneo la tukio.

Amesema bado haijafahamika hasa ni madhara gani yaliyotokea huko mpaka akifika eneo la tukio ambalo ni mwendo wa dakika 45 na atatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo eneo la ajali na madhara yaliyotokea.

Endelea kufuatilia Dar24 Media ili kujua undani wa taarifa hii.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 6, 2019
Mdude wa Chadema adaiwa kutekwa na wasiojulikana, Polisi watoa neno