Katibu mkuu wa chama cha mapunduzi (CCM), dkt. Bashiru Ally, amesema mchakato wa katiba mpya ni ajenda ya kudumu ya wananchi na haiwezi kufa licha ya kutekwa na wanasiasa wenye uchu wa kuingia ikulu.

Amebainisha hayo wakati akijibu shwali la mwandishi kuhusu mchakato huo wakati akipokea madiwani 11 wa chadema wa jiji la Mbeya waliohamia CCM jana.

Bashiru amesema kuna watu wanadhani ukiibua mchakato huo inalipa kama ilivyokuwa mwaka 2015.

” Ninawajua watu wavivu wa kufanya siasa za ushindani, wanatafuta viajenda hivi ambavyo vitawapa kiki. Hii ni ajenda muhimu lakini tumejadili tangu mika ya 1980 na hii katiba ya mwaka 1977 tumejadili sana na kuna mapinduzi makubwa yamefanywa ikiwemo kujumuisha haki za binadamu pamoja na mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Amesema jambo la katiba ni la wananchi lakini wanasiasa wanaligeuza kuwa jambo lao, lakini ajenda hiyo haiwezi kufa kwasababu ya wanasiasa.

RC Mtwara ataka kuboresha pombe ya gongo
Serikali yashusha rungu kwa madalali, usajili