Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetoa barua maalum ambayo inatoa taarifa kuwa Amber Ruth sio msanii hapa nchini, kwani hatambuliki na hajasajiliwa na Baraza hilo.

Kwa mujibu wa barua hiyo imeelezea kwamba iwapo Amber Rutty atafanya kosa lolote na kuvunja sheria, wahusika watamchukulia hatua stahili na halitajihusisha nae.

Sambamba na hilo barua hiyo imewaasa wasanii wote kufuata maadili na kutovunja shria za nchi, ili kutetea sanaa yao.

Amber Ruth amekuwa na skendo kubwa mara baada ya video zake akiwa faragha kuvuja mitandaoni, jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugol awalimtaka ajisalimishe polisi ndani ya masaa 12.

Historia za wachungaji 7 na utajiri wao
Auawa kwa kuoa mke wa pili bila kutoa taarifa

Comments

comments