Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) wamelifungulia Shindano la Miss Utalii Tanzania baada ya waandaaji kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa.

Maagizo yaliyotolewa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa ungozi na mfumo wa mashindano, ambapo tayari bodi ya mashindano imefanya mabadiliko hayo kwa kuanzisha ‘organisation structure’ ambapo sasa kuna ‘Governing Board’ na ‘Executive Board’ na ‘Management Team’.

Lakini pia wameanzisha mfumo mpya wa mashindano haya, ambapo sasa litakuwa shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania yaani Miss Tourism Tanzania International Ageant, ambalo washiriki kutoka duniani kote watawakilisha nchi zao kuwania taji la kimataifa la Miss Tanzania International.

Huku washirikï kutoka mikoa yote ya Tanzania wakiwakilisha mikoa yao katika fainali za kanda na hatimaye washindi wakiwakilisha kanda zao katika fainali za kimataifa wakiwanîa taji la Miss Utalii Tanzania yaani Miss Tourism Tanzania.

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 12, 2019
Waziri Mkuu achangia mifuko 300 ya sarufi ujenzi wa Kanisa la SDA Magomeni