Balozi wa China nchini Israel, Du Wei amekutwa akiwa amefariki dunia nyumbani kwake jijini Tel Aviv, leo, Mei 17, 2020.

Jeshi la polisi nchini Israel limesema limeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo. Lakini ripoti za awali zimeeleza kuwa Balozi Wei amekutwa na mfanyakazi wake akiwa amepoteza maisha kitandani kwake na kwamba mwili wake haukuwa na dalili zozote za kushambuliwa.

Balozi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 58, ameacha mke na mtoto mmoja. Aliteuliwa kuwa Balozi wa China nchini Israel Februari mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, Yuval Rotem amesema kuwa amezungumza na Naibu Balozi wa China nchini humo, Dai Yuming kumpa salamu za rambirambi. Amesema amemwambia kuwa Wizara hiyo itashirikiana na Ubalozi wa China kwa lolote watakalohitaji kuhusu tukio hilo.

Shirika la Huduma ya Kwanza la The Magen David Adom limeeleza kuwa chanzo cha kifo chake kinaonekana kuwa ni shambulizi la moyo.

JPM amtumbua Dkt. Ndungulile, amteua Dkt. Mollel

Waislamu watakiwa kuongeza ibada, kumi la mwisho

Mtoto wa Magufuli apona Corona kwa kujifukiza
Ndugu wanne wafariki kwenye tope wakimwokoa mwenzao

Comments

comments