Balozi Getrude Mongela amesema ni heri kumpigia kura mgombea mwanaume katika chaguzi mbalimbali kuliko mwanamke anayeona aibu kuzungumzika maendeleo ya wenzake.

Akizungumza jana katika mkutano uliwakutanisha viongozi wanawake nchini, Balozi Mongela amesema kuwa siku ambayo bunge litafikia asilimia 50 ya wanawake hatajali chama anachotoka mbunge ambapo amesema atajali mambo wanayozungumza.

”Kama mwanamke yeyote anaingia bungeni akiwa kama ameenda monyesho ya sabasaba ni heri nimpigie kura mwananume ni hasara kuwa na wanawake viongozi wanaoona aibu kuzungumza maendeleo ya wanawake” amesema Balozi Mongela.

Naye mwakilishi wa umoja wa Mataifa (UN) nchini hodan addou amesema kuwa mtandao wa wanawake Afrika tawi la Tanzania utazinduliwa ukiwa na malengo mbalimbali likiwemo kuwahimiza wanawake na viongozi wananwake kutimiza majukumu yao kuibadili Afrika.

Mwenyekiti mwenza wa mtandao huo Mary Rusimbi amesema mkutano huo unalenga kujiangalia , kujitathimini, kutafakari, uongozi wa mwanamke ulipo.

 

Katibu Bavicha ajivua gamba "Huu ndiyo mwisho wa chadema"
Iran: Naibu waziri wa afya aambukizwa Corona