Baba wa bondia Floyd Mayweather Jr, amekamatwa na Jeshi la Polisi la Las Vegas nchini Marekani akituhumiwa kumshambulia kwa masumbwi mwanamke mwenye umri wa miaka 59.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, mzee Mayweather anatuhumiwa kumpiga mwanamke huyo Septemba mwaka jana walipokuwa wanatoka kushuhudia pambano na masumbwi kati ya Canelo Alvarez na Gennady Golovkin.

Afisa wa jeshi hilo, Aden OcampoGomez amesema kuwa mwanamke huyo alifungua jarada Septemba 17 mwaka jana akieleza kuwa aliingia katika ugomvi wa majibishano ya maneno kati yake na mzee huyo katika eneo la maegesho ya magari ndipo alipomvuta kutoka kwenye gari lake na kuanza kumshambulia kwa masumbwi.

Mwanamke huyo alipelekwa hospitalini na akapatiwa matibabu ya majeraha hasa michubuko aliyoipata katika ugomvi huo.

Mzee Mayweather ambaye aliwahi kuwa mpiganaji wa masumbwi na sasa ni mkufunzi, alishikiliwa na jeshi hilo Jumatano wiki hii na aliachiwa kwa dhamana ya $1,000 akisubiri kupandishwa kizimbani Machi 27.

Endapo atakutwa na hatia kwa mujibu wa sheria, mzee huyo mwenye umri wa miaka 65 atakumbana na kifungo cha miezi sita jela.  

Video: Mbowe atema nyongo Siha, Jeshi la Polisi lamuwakia Kigwangalla
Ujumbe wa tambo za Lady Jay Dee wahusishwa na uamuzi wa Ruby