Mkazi wa mkoa wa Morogoro Wilayani Mvomero, Salehe Masokola (22), amewaua watoto wake watatu kwa kuwanywesha  sumu, kisha na yeye kutaka kujiua.

Mauaji hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, ambaye amesema tukio hilo lilitokea Novemba 27 ,mwaka huu saa sita mchana katika maeneo ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani. Kamanda Nyigesa amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mgogoro na mkewake na wakati ukitokea watoto walikuwa wakiishi kwa Bibi yao.

Baada ya mgogoro huo, mtuhumiwa alisafiri hadi kwa mkwe wake na kuwachukua watoto hao kuwa kudai anakwenda kucheza nao kisha baadae angewarudisha, aliwapakia watoto wake katika baiskeli kutoka Kunke hadi kitongoji cha Ditele Kibindu, Chalinze na akawanywesha sumu ya twiga, dawa ya kuulia magugu aliyoichanganya kwenye juisi ambayo ilipelekea kupoteza maisha papo hapo.

Kamanda Nyigesa ameeleza kuwa katika eneo la tukio wamekuta chupa mbili za Juisi zilizotumika, chupa ya dawa na matapishi ambavyo vilichukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Majina ya watoto waliofariki katika tukio hilo ni Shaila Salehe (6), Nurdin Salehe (4), na Sabrat Salehe aliye kuwa na umri wa miezi 10. na baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo na yeye aliamua kunywa Sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini ilishindikana kwakuwa aliokolewa na wasamalia wema na kupelekwa Hospitali  ya Mission ya Bwagala ambako anaendelea na matibabu chuni ya uangalizi wa Polisi japo haliyake bado ni Mahututi.

Video: Chanzo Mbowe na Matiko kurudi tena mahabusu, Burundi 'yavunja' kikao marais EAC
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 1, 2018