Rais wa Jamhuri ya Muungaano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya January Makamba.

Uteuzi huo wa Rais Magufuli unamfanya Simbachawene kuweka rekodi ya kuwa Mbunge pekee ambaye alitenguliwa kwenye Baraza la Mawaziri na kurejea tena baada ya miaka miwili iliyopita.

Septemba 06. 2017 akiwa Waziri wa TAMISEMI, Simbachawene alitajwa kwenye ripoti ya Uchimbaji wa madini ya Tanzanite, na Almasi kupitia Kamati ya Bunge, ripoti ambayo iliwasilishwa kwa Spika Ndugai na yeye kumkabidhi Waziri Mkuu Majaliwa ili aipeleke kwa Rais Magufuli.

aIdha, Septemba 06. 2017 baada ya ripoti hiyo kukabidhishwa kwa  Rais Magufuli, Simbachawene alitangaza kujiuzulu nafasi Uwaziri wa TAMISEMI ili kupisha tuhuma dhidi yake.

Agosti 28, 2018, Simbachawene alichaguliwa na Wabunge wenzake kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Ghasia ambaye alitangaza kujizulu,

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 22, 2019
Video: Urais unavyoitesa CCM, Lissu aingia"Vitani" rasmi