Baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa Andy Ruiz, bondia Anthony Joshua ameshauriwa kumtimua kocha wake, Rob McCraken kwani ni mtu wa daraja la tatu.

Ushauri huo umetolewa na bondia wa zamani wa uzito wa juu na bingwa wa dunia, Lennox Lewis ambaye amemwambia Joshua kuwa aachane na mwalimu wake ambaye anamfundisha, baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Andy Ruiz.

Kocha McCracken amekuwa kocha wa Joshua kwa muda mrefu sasa huku akimsaidia kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa IBF, WBA na WBO, lakini Lewis anaamini anapaswa kuachana na mwalimu huyo hasa kutokana na matokeo hayo yaliyo muaibisha aliyoyapata kwenye ukumbi wa Madison Square Garden mwishoni mwa wiki iliyo pita.

“Ninasema huwezi kwenda duniani huku ukiwa na mwalimu wa daraja la tatu, huwezi kuwa na jibu la maswali yako kwa daraja unalolitaka, anahitaji kuwa na profesa, McCracken ni mwalimu lakini kwa sasa Joshua hawezi kuendelea kuwa chini yake kwa sababu daraja lake ni la chini” amesema Lewis.

Na amesisitiza kuwa hadhani kama kuna umuhimu wa  bondia Joshua kuendelea kuwa na mwalimu ambaye kiwango chake kipo chini.

 

Rihanna ndiye mwanamuziki millionea wa kike Duniani
Kundi la waasi la ADF laua watu 12 DRC

Comments

comments