Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, Hamisi Mandi aka B12 amefunguka jinsi anavyokikubali kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Omary ‘Lil Ommy’ Tambwe.

Akifunguka kupitia ‘Nje ya Box’ inayopatikana kwenye Afropods inayowekwa mtandaoni (afropods.com), B12 ambaye anatajwa kuwa mtangazaji bora zaidi wa vipindi vya burudani Afrika Mashariki, alisema kuwa nje ya Clouds FM, The Playlist ni kipindi bora zaidi cha redio.

“Nje ya Clouds Media, kipindi ninachopenda kukisikiliza… the playlist ya Lil Ommy is the best radio show (ni kipindi bora zaidi cha redio),” amefunguka.

The Playlist ambayo ilikuwa ikisikika mara moja kwa wiki kupitia 100.5 Times Fm, juzi ilifanya mabadiliko na kuzindua msimu mpya ambapo itakuwa ikisikika kila siku za wiki kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

Akizungumza na Dar24 kuhusu kauli ya B12, Lil Ommy alisema kuwa hiyo kwake ni heshima kubwa.

“Kwangu hii ni heshima kubwa sana, ni ‘privilege’ inayonipa nguvu zaidi ya kufanya kazi. Kwa sababu B12 ni mtangazaji wa muda mrefu, mkubwa na mwenye heshima kwenye game na watu wote tunajua hilo. Ameibua vipaji vingi. Hii mimi ninaipokea kwa mikono miwili,” Lil Ommy aliiambia Dar24.

Aliongeza kuwa amekutana kwa mara ya kwanza na B12 katika tuzo za MTV MAMA nchini Afrika Kusini na kuzungumza naye na kupata picha ya pamoja. Hivyo, anashauri watu walio kwenye tasnia ya utangazaji kushirikiana na kupeana moyo pale inapobidi.

“Hii inanipa nguvu sana, inakufanya uone kuna kitu ambacho unafanya na watu wanaona na wanakubali kwahiyo niweze kuongeza zaidi ya vile ambavyo ilikuwa ikifanyika.

B12 na Lil Ommy

“Shout Out kwa B12 for the love and support (kwa upendo na kuniunga mkono), tuko katika tasnia moja tunaonana kwenye mitandao na tunakutana sehemu kadhaa so tuko pamoja. Kweli jamaa ‘you’re born to shine’ (ulizaliwa kung’aa),” aliongeza.

Wizara ya Ardhi yabuni mbinu mpya za ulipaji kodi pango la ardhi
Video: Kenyatta, Odinga mchuano mkali, Waliopiga mabilioni viwanda kitanzani