Uongozi wa Azam FC umesema hauna tatizo na uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumbadilisha mwamuzi wa mchezaji wa Ngao ya Jamii, Jumamosi.

Mchezo huo unawakutanisha Azam FC dhidi ya Yanga ambao utarushwa moja kwa moja na runinga ya Azam TV, sasa utachezeshwa na Martin Saanya.

TFF imembadilisha Israel Nkongo ambaye ameelezwa kuwa na matatizo ya misuli.

Katibu wa Azam FC, Idrissa Nassor amesema wao wanachotaka ni uchezeshaji wa kufuata sheria 17 za soka.

“Kwa kweli hatuna tatizo, kama sheria 17 za soka zitafuatwa sisi hatuna tatizo.

“Hiyo si kazi yetu, kikubwa ni maandalizi ambayo tumekuwa tukiendelea kuyafanya,” alisema Nassor.

Mrema Akiri Nguvu Ya Lowassa Ni Zaidi Yake Mwaka 1995
Balotelli Hataki Kurudi Italia