Klabu ya  Azam FC, sasa imetoa fursa kwa mashabiki wa timu hiyo kuwatunuku tuzo wachezaji wao pendwa kila mwezi wakati wa mechi za mashindano.

Tuzo hizo ni maalumu kabisa huku zikiwa chini ya udhamini wa Benki ya NMB ambao ni wadhamini wakuu wa timu hiyo na Tuzo hizo zitakwenda kwa jina la ‘NMB Player of the Month’ zitakazo kuwa zikitolewa kila mwezi kwa mchezaji bora aliyefanya vizuri kwa mwezi husika.

Azam FC kwa kuanza rasmi mchakato, wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa imeanza rasmi Agosti 26 kwa Azam FC kuichapa Ndanda bao 1-0, sasa Azam wanakupa fursa ya kumchagua mchezaji bora wa mwezi huo uliopita.

Tuzo hiyo ya kwanza itatolewa wiki ijayo Septemba 23 mwaka huu, kabla ya kuanza mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Lipuli utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 1.00 usiku.

Hata hivyo, Ujio wa tuzo hizo haujaiacha mbali timu ya vijana ya Azam FC (Azam FC U-20), kwani nao watatunukiwa kila mwezi kama ilivyo kwa timu kubwa huku tuzo za Azam B zikiwa zinadhaminiwa na Maji safi ya Uhai na zitakua na jina lake ambapo zitaitwa ‘Uhai Player of the Month.’

Hodgson aanza kwa kipigo Crystal Palace
Linah: Sikuwa tayari Kuzaa

Comments

comments