Hatimae mshambuliaji kutoka nchini Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ametangaza hadharani kuwa tayari kuihama Borussia Dortmund kabla ya kufungwa kwa diridha la usajili, mwishoni mwa mwezi huu.

Aubameyang amekua akihusishwa na mipango ya kuwaniwa na klabu za Chelsea na AC Milan, huku aliekua meneja wake Jurgen Klopp anaekinoa kikosi cha Liverpool kwa sasa, akitajwa kuwa miongoni mwa wanaoitamani huduma ya mshambuliaji huyo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameweka wazi mpango wa kutaka kuihama BVB, alipohojiwa na kituo cha Radio cha Montecarlo.

“Bado nina malengo ya kucheza soka, lakini itanipendeza nikiwa na klabu nyingine tofauti baada ya dirisha la usajili kufungwa.

“BVB ni klabu nzuri, ina mashabiki wanaojali, lakini naamini imefikia muda wa kubadilisha mazingira ya soka langu, naamini itawezekana kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili juma lijalo.” Alisema Pierre-Emerick Aubameyang

Mwishoni mwa juma lililopita mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Michael Zorc, alitangaza hawatokua tayari kumuuza mshambuliaji huyo katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Video: Mnanionea tu kuninyang'anya mashamba yangu - Sumaye
Justine Bieber avunja urafiki na Mayweather kisa ‘Upako’