Watu sita Mkoani Kagera wameuawa katika matukio tofauti tofauti akiwemo, Colletha Francis mwenye umri wa miaka 65 mkazi wa kijiji cha Ihunga kata Kishanda wilaya ya Muleba mkoani humo, aliyeuawa na wananchi wenya hasira kali baada ya kumtuhumu kuhusika na mauaji ya mtoto Ismail Hamisi mwenye umri wa miaka 7, ambaye baada ya kuuawa aliondolewa sehemu zake za siri.

Kufatia tukio hilo la kusikitisha mkuu wa wa wilaya Muleba Mhandisi, Richard Ruyango amesema kuwa amesikitishwa na tukio hilo ambapo amewataka wananchi wa kata ya Kishanda kuhakikisha wanawataja wale wote waliohusika na mauaji hayo.

Amesema kuwa kumekuwa na kukithiri kwa vitendo vya mauaji yanayosababishwa na wananchi kujichukulia hatua mikononi suala ambalo linahatarisha amani katika jamii na kuwahakikishia wananchi kuwa serikali itahakikisha hali ya usalama na utulivu inakuwepo muda wote.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa, baada ya mtoto huyo aliyeondoka nyumbani akielekea shule tangu Aprili 05 mwaka huu kugundulika kuwa ameuawa na kuzikwa karibu na makazi ya bibi huyo, wananchi walimvamia nyumbani kwake na kuanza kumshambulia, na kisha kuchoma moto nyumba yake na kufyeka mazao ikiwemo migomba na mibuni, ambapo mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa akihusishwa na tukio hilo.

Kamanda Malimi amesema kuwa tukio la mauaji ya mtoto huyo ambaye baada ya uchunguzi alizikwa, linahusishwa na masuala ya kishirikina, kutokana na kugundulika kuondolewa baadhi ya viungo vya mwili wake.

Aidha, Kamanda Malimi amewataja wengine waliouawa kuwa ni MG.433651 Steven Sospeter askari mgambo mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Gera wilayani missenyi aliyefariki dunia akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na kikundi cha bodaboda baada ya kutuhumiwa kuiba pikipiki, Adela Eliud mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji cha mlela aliyekutwa ameuawa na mume wake.

Wengine ni Karim Abdallah mwenye umri wa miaka 18 Mrundi na Razalo Silvanus mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa kitongoji cha ngoma wilayani Muleba ambapo wote wameuawa kwa tuhuma za ujambazi.

Nyoka weusi wamuondoa Rais Weah ofisini, wapotea
Sudan: Waandamanaji watangaza kung'oa utawala wa Kijeshi, kusimika wa Kiraia