Kijana mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 17 ambaye ana ulemavu wa ngozi amekutwa akiwa ameuawa na ubongo wake kuchukuliwa huko nchini Msumbiji

Aidha, mkazi wa eneo la Tete, Magharibi mwa Msumbiji, ambaye hakutaka jina lake kutajwa, amesema kuwa wazazi wa mvulana huyo walianza kumtafuta mara baada ya kutoweka nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) zinasema kuwa mwili wa kijana huyo ulipatikana ukiwa hauna mikono na miguu huku kichwa chake kikiwa kimepasuliwa na ubongo wake kutolewa

Msemaji wa jeshi la polisi wa mkoa wa Tete, Lurdes Ferreira amesema kuwa polisi wataanzisha uchunguzi katika eneo ambalo mauaji hayo ya kinyama yametokea ili kuweza kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo.

Hata hivyo, tukio hilo ndilo tukio la karibuni zaidi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao mara kwa mara hushambuliwa kwa sababu ya ushirikina huku wakidai kuwa viungo vyao vinaweza kuleta utajiri.

Serikali kukomesha biashara ya ngono
Video: Majaliwa awaasa watendaji wa taasisi zinazosimamia mazao ya biashara