Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela aliyekuwa Mhasibu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Gryson Mnyawami baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa zaidi ya Sh9 milioni akiwa mtumishi wa umma.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashtaka ambao walithibitisha wizi huo pasipo kuacha shaka.

Aidha, Wakili wa Serikali Janeth Magoho ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa huyo ni mkosaji wa kwanza na hakuna kumbukumbu za makosa mengine.

Hata hivyo, Magoho aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo kwa kuwa kitendo cha wizi alichofanya akiwa mtumishi wa umma ni kibaya na kinaitia hasara Serikali.

Boubacar Keita ashinda tena kiti cha Urais Mali
DC Ole Sabaya amsweka ndani mwekezaji shamba la Kibo