Mahakama kuu kanda ya Kigoma imemhukumu kulipa faini ya shilingi laki tatu, Msafiri Ntarakila (68), mkazi wa kijiji cha Kasulu mkoani Kigoma kwa kosa la kumuua mke wake kwa kipigo, Agosti 15, 2018.

Akisoma maelezo ya kesi hiyo wakili wa Serikali, Happy Mayunga amedai mshtakiwa alitenda kosa hilo usiku baada ya kurudi nyumbani kwake akiwa amekunywa pombe na kukuta mke wake akiwa hayupo nyumbani.

Mayunga amedai mshtakiwa baada ya kumkosa mke wake alimtafuta na kumpata ndipo alipoanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili hatua iliyosababisha kuvuja damu nyingi na alifariki alipokuwa njiani anapelekwa hospitali.

Awali Jaji mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Kigoma, Ivin Mugeta anayesikiliza keshi hiyo alipomhoji mshtakiwa kuhusu kuhusika na tukio hilo, mshtakiwa alikiri kutekeleza mauaji hayo.

Kutokana na upande wa mashtakiwa kukiri kosa, upande wa jamhuri uliomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kama funzo kwa mshtakiwa na jamii.

Wakili wa upande wa utetezi aliomba mahakama kupunguza adhabu kwa mshtakiwa kutokana na kosa hilo kuwa la kwanza, mazingira ya kosa kuonesha si ya kukusudia, umri wake kuwa miaka 68 pamoja na kutegemewa na familia ya wajukuu watano.

” Nimezingatia utetezi wa kosa ulilolifanya na umri ulionao hivyo mahakama hii inakuhukumu kulipa faini ya shilingi laki tatu kama utapata na ukikosa basi utatumikia jela miaka mitatu” alihitimisha Jaji Mgeta.

Siku 18 zabadili upepo wa Emre Can
Casillas atia nia urais RFEF