Kipindi cha ujauzito ni wakati wa kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha ya mjamzito. Moja ya mambo makubwa ni pamoja na tabia ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mjamzito hashauriwi kuvaa viatu vyenye visigino virefu kutokana na athari zinazoweza kutokana na aina hizi za viatu, kama ifuatavyo.

Maumivu ya misuli ya mapaja.
Wadada hupenda kuvaa “high heels” husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.

Maumivu ya mgongo.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.

Hatari ya kuanguka.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa “high heels” na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.
Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.

Mimba kutoka.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.

Lakini, iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo

Ni salama kuvaa viatu hivi katika muhula wa kwanza wa ujauzito (Miezi mitatu ya mwanzo), viatu visiwe virefu sana na visigino viwe imara, lakini pia inapaswa kuvaa viatu visivyo na bugdha na visikaze sana.

Ni vyema kuepuka visigino vyembamba sana na si siku nzima vitoe mara kwa mara kupumzisha miguu.

Na epuka kutembea au kusimama muda mrefu ukiwa umevivaa endapo utahisi maumivu kwenye misuli ya mapaja jaribu kufanya mazoezi ya kujinyoosha na kujikanda.

Askofu Gwajima akutana na JPM Ikulu, afunguka 'lazima uvunje mayai'
Marekani kuchunguza taarifa za mitandao ya kijamii za wanaoomba VISA