Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi, kupandikiza chuki za ubaguzi wa kikabila na kusema kuwa dhambi ya kubaguana na dhambi ya watu wenye nafasi kuwakanyaga wengine ni moja ya dhambi kubwa ambazo binadamu anatakiwa kuomba toba kwa Mungu.

Askofu Dk. Shoo ametoa kauli hiyo, wakati akiendesha ibada ya sala ya maombi ya aliyekuwa mwenyekiti wa makampuni ya IPP Limited, Dk. Reginald Mengi.

“Kama kuna dhambi ambayo tunapaswa kujutia na kutubu, ni dhambi ya ubaguzi. Tusiruhusu watu kutuingiza kwenye dhambi hiyo,” alieleza Askofu Dk. Shoo.

Ameongezea kuwa viongozi vijana wa kisasa wanajifanya wajuaji wanajitutumia amewasihi kutulia na kujishusha kwani wasipojishusha Mungu atawashusha.

”Viongozi wenye umri mdogo muache kujitutumua kama kifutu, tuwe kama Mengi, licha ya uwezo wake alikuwa akijishusha na kuwasaidia wote, Kila siku huwa nasakli kwa ajili ya viongozi, msipojishusha Mungu atawashusha” amesema Askofu Shoo”amesema Askofu Shoo.

Askofu Shoo amesema hayo baada ya kutokea kwa msiba wa Mengi kuna watu walianza kuweka machapisho katika mitandao ya kijamii na kuanza kuhukumu na ameomba watu kuendelea kumenzi mazuri yaliyokuwa yakifanywa na Dk Mengi enzi za uhai wake.

Mbowe akemea kauli za ubaguzi
LIVE: Mazishi ya Dkt. Reginald Mengi Machame - Kilimanjaro