Askari wa kike wa jeshi la polisi nchini Kenya anayefanya kazi katika eneo la Kericho ameripotiwa kujipiga risasi kwa kutumia bunduki aina ya AK 47 na kujiua kufuatia ubishani uliozuka kati yake na mpenzi wake.

Mmoja kati ya viongozi wa jeshi hilo katika eneo hilo amekiambia kituo cha runinga cha Citizen kuwa mpenzi wa marehemu ambaye ni mfanyakazi wa kitengo cha Hifadhi ya Wanyama Pori, alifika kwa marehemu kumtembelea lakini walianzisha ubishani.

Ameeleza kuwa marehemu ambaye siku hiyo alikuwa katika zamu ya usiku kazini, alienda kituoni na kuchukua bunduki aina ya AK47 na kisha kujipiga risasi.

Mwili wake umeondolewa na jeshi la polisi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kapkatet.

Chanzo cha ubishani wao bado hakijawekwa wazi, kwa mujibu wa Citizen.

Prof. Mbarawa anena kuhusu vichwa 11 vya Treni
Video: Deontay Wilder amshikisha adabu Ortiz, amvimbia Anthony Joshua