Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu.

Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililotokea Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, akiwa Makao Makuu ya UN, Mjini New York Desemba 22, 2017 usiku.

Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana na msiba huo.

Safari za usiku zapigwa marufuku
Video: Mwalimu asimulia mateso ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji mara kumi