Askari wa Jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), Michael Hosea mkoani Tabora amejiua kwa kujipiga risasi mara nne baada ya kuchukua bunduki katika ghala la silaha kuelekea lindo la Acces Bank.

Katika taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoani huko, SACP Wilbroad amesema askari huyo alijiua mapema leo hii majira ya saa 11:45 alfajiri.

Aidha kamanda huyo amesema watu wengi wenye tabia ya kujiua ni wale wenye tabia za ndani kwamba watu wa aina hiyo hupatwa na matatizo lakini wanashindwa kuyaeleza kwa watu wao wa karibu hivyo hujikuta kuishia kunung’unika ndani ya nafsi zao matokeo ya tabia hiyo ni kujichukulia hatua mkononi ikiwa ni pamoja na kujiua.

”Leo alfajiri majira ya saa 11:45 askari wetu namba G8845 DC Michael Hosea wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Tabora, alijiua na kujipiga risasi baada ya kuchukua bunduki katika ghala la silaha katika tayari kuelekea kwenye lindo la Acces Bank”. SACP Wilbroad.

Ameongezea kuwa ” sasa watu wengi wenye tabia za kujiua wenye maamuzi ya kuchukua hatua mkononi na kutoa maisha ya ni waty wenye tabia za ndani ”Introvat behaviour” akiwa na tatizo hawezi kumweleza mtu, yani ananung’unika ndani ya nafsi yake na kutoa maamuzi ndani ya nafsi yake” amesema Kamanda huyo”.

 

Video: Mtanzania aliyehitimu kidato cha 6 avumbua roboti la mkono kwa walemavu
Tanzia: Mke wa Kibonde afariki dunia

Comments

comments