Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia hakimu wake, Vick Mwaikambo imewahukumu askari sita akiwemo wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Sh 500,000 na madumu 109 yenye mafuta kila mmoja baada ya kukiri shtaka la wizi wa mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik).

Askari hao ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza.

Mwaikambo amesema kwa kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza hivyo mahakama hiyo imewapa adhabu hiyo.

Awali wakili wa Serikali Mwandamizi, alidai kuwa washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu hivyo walikubaliana kuliondoa shtaka la kwanza la kupanga genge la uhalifu na shtaka la tatu la utakatishaji wa fedha na kuwashtaki kwa shtaka la pili la wizi.

Julai 30, mwaka huu washtakiwa hao katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam, waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh 4,647,760 mali ya ATCL.

Video: JPM abariki bakora za RC, Jinsi msajili anavyoweza kumchomoa Mbowe
Ujenzi wa machinjio Vingunguti usiku na mchana, wamvuta Waziri