Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, inawachunguza askari polisi sita wa Kituo cha Igunga kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh milioni 8 kwa mkazi wa Kijiji cha Isakamaliwa, Ngaka Mataluma (95) ili wasimpeleke kituoni.

Inadaiwa kuwa Juni 12, mwaka huu, askari hao walikwenda kwa Mataluma na kuomba Sh milioni 20, lakini wakajadiliana hadi Sh milioni 8.

Askari hao ni Inspekta Frank Matiku, PC Raphael Maloji, D.1 Koplo Paul Bushishi, PC Lome Laizer, DC Lucas Nyoni na Koplo Charles ambao wote wanafanya kazi Kituo cha Polisi Igunga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusisitiza kuwa wenye nafasi ya kulizungumzia vizuri suala hilo ni Takukuru ambao ndio wahusika zaidi na masuala ya rushwa.

“Suala hili nimelisikia, wenzetu wa Takukuru ndio wanaohusika zaidi na masuala ya rushwa, watafuteni, sisi tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwao, tutachukua hatua,” alisema Kamanda Nley.

Mmoja ya mkazi wa kijiji hiko katika kikao kilichoitishwa na Diwani wa kata ya Isakamaliwa kama hatua mojawapo ya kujadili rushwa kijijin hapo amesema siku iliyotokea tukio hilo naye pia alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi ambapo aliambiwa anajihusisha na upigaji ramli chonganishi tuhuma ambazo alikataa katakata na kuamriw akutoa shilingi milioni nne, ambapoa alisema hana kiasi hiko cha pesa na kumlazimisha atoe shilingi laki 5, moja wa kijana wake aliamua kumtolea shilingi 450,000 ili aachiwe huru.

Hata hivyo kesi hiyo tayari ipo mikononi mwa Takukuru hivyo wanaifanya kazi na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

 

 

Vita ya Nicki Minaj na Miley Cyrus yafika pabaya
Wema Sepetu atoka rumande, apewa onyo la mwisho