Unaweza kuita janga ama tetemeko la elimu nchini Uganda lililobainika kupitia utafiti uliofanywa hivi karibuni na Serikali ya nchi hiyo uliobaini kuwa asilimia 80 ya walimu wa shule za msingi walioajiriwa mwaka jana hawajui kusoma na kufanya hesabu rahisi.

Matokeo hayo yametokana na utafiti uliowalenga walimu wa shule za msingi waliohitimu mafunzo ya ualimu mwaka 2015, kwa lengo la kutaka kuthibitisha madai ya uozo wa mfumo wa elimu ya msingi nchini humo.

Kwa mujibu wa Daily Monitor, Katibu Mkuu wa Bodi ya Mitihani ya Uganda, Daniel Odongo amethibitisha matokeo ya utafiti huo akiongeza kuwa imebainika pia asilimia karibu 80 ya wanafunzi wa mwaka wa pili katika vyuo vya walimu wa shule za msingi hawana uwezo wa kufanya hesabu rahisi na kusoma kiingereza.

“Ni asilimia 21.8 tu ya wanafunzi wa vyuo vya walimu wa shule ya msingi (wanaoandaliwa kuwa walimu) ndio wana uwezo wa kufanya mahesabu rahisi, na asilimia 38.8 tu ndio wanaoweza kusoma na kuandika kiingereza,” alisema Odongo.

gazeti-la-daily-monitor-2-jpg-large

Odongo alieleza kuwa matokeo hayo yanatoa ishara kwa Serikali kulitatua tatizo hilo mapema iwezekanavyo ili kuokoa jahazi la elimu ya msingi nchini humo.

Waziri wea Elimu ya Msingi, Rosemary Sseninde amesema kuwa hakuna mtu yoyote atakayejiunga na ualimu wa msingi kama atashindwa kufaulu masomo ya hisabati na kiingereza.

Takribani zaidi ya watanzania 9 wanapoteza maisha ndani ya siku moja kwa ajali barabarani.
Serengeti Boys Yaenda Kigali - Rwanda

Comments

comments