Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameripotiwa kutengana na mkewe aitwae Annie.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la nchini England, babu huyo mwenye umri wa miaka 65 amelazimika kutengana na mkewe kutokana na maamuzi yaliyotolewa na mahakama jijini Paris nchini Ufaransa.

Amri ya mahakama imetolewa siku za hivi karibuni na imemtaka Arsene kuendelea kumuhudumia mwanamama huyo ikiwa ni pamoja na kugawana mali zisizohamishika na zile zinazohamishika.

Pamoja na yote hayo kutokea wawili hao tayari walikua wameshazaa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 18, ambaye atakua na uhuru wa kuchagua aishi na nani katika kipindi hiki kutokana na umri wake kumruhusu kufanya lolote.

Balaa lililosababisha ndoa ya Wenger kuvunjika linatajwa kuwa ni mahusiano ya kimapenzi yaliyokua yakiendelea kati yake na msanii wa muziki wa kufoka nchini Ufaransa aitwae Sonia mwenye umri wa miaka 39.

Mahusiano hayo yalibainika siku chache kabla ya Arsene Wenger hajafunga ndoa na Annie mwaka 2010, baada ya kuishi nae kwa muda mrefu kama rafiki yake ya kike.

Robert Lewandowski Aushangaza Ulimwengu
Angelina Jolie Na Brad Pitt Waongeza Mtoto Kutoka Syria