Klabu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza, Arsenal imekaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji matata kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Klabu ya Borussia Dortmund kwa karibu £60m.

The Gunners tayari walikuwa wamewasilisha maombi ya kutaka kumchukua Aubameyang mara mbili lakini yakakataliwa na Dortmund.

Klabu ya Dortmund imesema kuwa wako tayari kumuuza mchezaji huyo endapo vipengele fulani muhimu vitatimizwa kikamilifu.

“Tuko tayari kukamilisha uhamisho lakini ikiwa matakwa fulani yatatimizwa kikamilifu, msimamo wetu uko wazi kwa Klabu ya  Arsenal kwakuwa wamefanya majaribio kadhaa mpaka kufikia sasa, lakini tumeyakataa yote,”amesema mkurugenzi wa michezo Michael Zorc

Hata hivyo, Arsenal wanamtafuta kwa udi na uvumba, Aubameyang ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mchezaji wa Chile, Alexis Sanchez aliyejiunga na Manchester United mapema mwezi huu kwa kubadilisha na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan.

Gumzo: Diamond amtuliza Wema kifuani hadharani
Mtaa wateketea kwa moto jijini Nairobi