Kamanda wa polisi Mkoani Manyara Augustino Senga, amethibitisha kuuwawa kwa mfanya biashara Josephine Everest (38), mkazi wa Nyungu aliyekutwa akiwa amenyongwa kwa sweta , chumbani kwake.

Ameeleza kuwa mauaji hayo yaligundulika Novemba 26, mwaka huu, saa tatu asubuhi,mataa wa Nyungu wilayani Babati, Mkoani Manyara, ambapo mwili wa mwanamke huyo, uligundulika chumbani kwake ukiwa umenyongwa kwa kutumia sweta la mume wake, aitwae Baraka Mollel.

Kwamujibu wa Kamanda Senga amesema kuwa mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumnyonga mkewe kwa kutumia sweta kitandani na baada ya kuhakikisha amefariki, alitoka nje na kufunga mlango kwa kitasa na kutokomea kusiko julikana, Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 23, mwaka huu ambapo marehemu aliwasiliana kwa mara ya mwisho na watoto wake ambao wanalala chumba kingine kwenye nyumba ya kupanga.

Hofu ya awali ya kuuwawa kwa marehemu Josephine iliwapata nduguze baada ya mdogo wa marehemu kupokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa marehemu usemao”Baba Isack amenipiga” ndipo akaelekea nyumbani kwa dadayake na alipofika akakuta mlango umefungwa, aliamua kutoa taarifa Polisi ambao walichukua jukumu la kuvunja mlango na kumkuta marehemu amefariki dunia huku shingoni amefungwa kwa kutumia sweta.

Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika, lakini uchunguzi wa awali unaonesha marehemu alikuwa kwenye mgogoro na mumewe, uliochangiwa na ulevi wa pombe wakati mke alikuwa akimkataza mumewe kulewa, Kamanda Senga amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi watukio hilo, ikiiwemo kumsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye inadaiwa amekimbilia Arusha.

Video: Thabo Mbeki amvulia kofia Magufuli, ukaribu wa Magufuli na Lowassa wafikirisha
Mbatia amshtaki Warioba kwa JPM

Comments

comments