Mkazi mmoja Mkoani Njombe amenusurika kifo mara baada ya kujaribu kujiua kwa kunywa sumu baada ya kushindwa kurejesha michango ya wanachama inayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi laki sita.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Rashid Ngonyani ambapo amesema kuwa binti huyo, Maria Mgeni (26) mfanyabiashara ndogo ndogo wa mboga mboga alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ambayo bado haijajulikana pamoja na kujichana maeneo ya kitovuni kwa kitu chenye ncha kali.

Kamanda Ngonyani amesema kuwa binti huyo ambaye ni muweka hazina aliamua kufanya hivyo kwa nia ya kukwepa kulipa deni ambalo alikuwa anadaiwa ili aweze kuwasilisha katika kikundi chake.

“Huyu mwanadada anacheza mchezo wa kupeana shilingi 2000 kila siku na huu mchezo una wanachama takribani 90 kwa hiyo yeye alikuwa ni muweka hazina wa chama chao na tarehe hiyo aligundulika hajawasilisha baadhi ya michango ya wanachama wake inayokaribia laki sita kwa hiyo alifanya hivyo kwa nia ya kukwepa kulipa deni ambalo alikuwa akidaiwa ili aweze kuwasilisha, na mtuhumiwa mpaka sasa anashikiliwa na polisi na upelelezi unaendelea,”amesema Kamanda Ngonyani

Adha, Kamanda Ngonyani amesema kuwa jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia mkazi mmoja wa mtaa wa Matalawe aliyefahamika kwa jina la Zebedayo Mgulunde (23) fundi ujenzi kwa kosa la kujaribu kujiteka.

Hata hivyo, kuhusu matukio ya mauaji ya watoto wadogo yanayoendelea mkoani Njombe, Ngonyani amesema kuwa jeshi hilo mpaka sasa linawashikilia watuhumiwa wawili wanaojihusisha na matukio hayo huku akimtaja Joel Joseph Nziku (35) ambaye ni dereva pamoja na Alphonce Edward Danda (51) Mkazi wa Makambako wote wakihusishwa na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto.

Aliyeikataa kesi ya Zitto kuhusu CAG asifiwa na CJ
Zengwe laibuka mgao wa fedha za Tasaf