Hatimaye mabingwa wa soka nchini England, Chelsea wamemtangaza rasmi kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte kuwa meneja wa kikosi chao kuanzia msimu ujao.

Chelsea wamemtangza Conte, baada ya kukamilisha taratibu za kusaini mkataba wa miaka mitatu, zilizofanyika jana magharibi mwa jijini London, wenye thamani ya Pauni Milioni 20.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, alipata umaarufu alipokuwa anaifundisha klabu bingwa nchini Italia, Juventus kabla ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia.

Conte, anatarajiwa kuhamishia mafanikio yake Stamford Bridge, baada ya Chelsea kupitia msimu mbaya zaidi tangu inunuliwe na taykun kutoka nchini Urusi, Roman Abramovich.

Dau lake linahusisha mshahara wa Pauni Milioni 6.5 na posho ya Pauni Milioni 5 akishinda taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Lakini jukumu lake la kwanza na kuipeleka klabu katika michuano ya Ulaya.

Kwa sasa Chelsea ipo chini ya meneja wa muda kutoka nchini Uholanzi, Guus Hiddink aliyepewa timu amalizie msimu baada ya kufukuzwa kwa Jose Mourinho, mwishoni mwa mwaka jana.

Conte anaendelea kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Italia ambacho kitakua na jukumu la kupambana katika fainali za kombe la mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016), zitakazofanyika nchini Ufaransa kuanzia Juni 10 hadi Julai 10 mwaka huu.

WASIFU WA ANTONIO CONTE  

Mataji Aliyoshinda Akiichezea Juventus

Serie A: 1995, 1997, 1998. 2002, 2003

UEFA Cup: 1993

Ligi ya Mabingwa: 1996

Mataji Aliyoshnda Akiwa Kocha

Juventus: Serie A (2012, 2013, 2014)

Bari: Serie B (2009)

Historia Yake Ya Ukocha

Arezzo: 2006 – 2007

Bari: 2007 – 2009

Atalanta: 2009- 2010

Siena: 2010- 2011

Juventus: 2011 – 2014

Italia: 2014-2016

Wanaosakwa kwa wizi wa mabilioni Uingereza waishi Tanzania kwa utulivu
Mussa Kisoky: Tumebariki Adhabu Za Waliopanga Matokeo