Hatimaye mbabe wa masumbwi duniani, Anthony Joshua amekubali kumpa pambano moja Tyson Fury baada ya kushuhudia matokeo ya sare kati ya bondia huyo na Deontay Wilder, wikendi iliyopita.

Uamuzi huo wa A. Joshua umekuja kufuatia kauli nyingi za mashambulizi dhidi yake kutoka kwa Fury, ambaye baada ya pambano lake alidai kuwa Joshua ni muoga akimfananisha na kifaranga.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Joshua alianza kwa kumsifu Fury ambaye ni Muingereza mwenzake kwa jinsi alivyoweza kupita kwenye pambano hilo.

“Anyway, kazi nzuri Fury. Walitaka kukuchukua wewe kwa sababu walidhani kuwa umekwisha. Nitakupa pambano moja utakapokuwa tayari,” ameandika Joshua. “Nitampa mmoja kati yenu nafasi [kati ya Wilder na Fury]!”

Deontay Wilder akijaribu kumrushia konde Tyson Fury katika pambano lao la Desemba 1 kuamkia Desemba 2.

Hii ilimaanisha kuwa ingawa Joshua ameonesha kumuunga mkono zaidi Fury ambaye ni Muingereza mwenzake, amempa nafasi pia Wilder ambaye watu wengi walitaka apande naye ulingoni.

Fury na Wilder wamekuwa wakitamba kuwa Anthony Joshua anawakwepa na kwamba anachagua watu wa kupigana nao. Wilder amekuwa akidai kuwa timu ya Joshua inapotezea mpango wa pambano kati yao kwakuwa wanaogopa.

Calisa aibuka kidedea mashindano ya Mr. Afrika
Video: Bulaya amjia juu Kigwangallah, 'Huu ni unafiki'

Comments

comments