Klabu ya AC Milan, imethibitisha itamkosa kiungo Andrea Bertolacci katika mchezo wa ligi ya nchini Italia wa mwishoni mwa juma hili baada ya kuumia paja akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa.

AC Milan wamelazimika kutoa taarifa hizo kufuatia joto la mchezo utakaowakabili dhidi ya Inter Milan kuendelea kupanda miongoni mwa mashabiki wa soka wa mjini Milan, kwa kuamini mambo yatakua magumu kwa kila upande.

Bertolacci, aliondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Italia na kurejeshwa klabuni kwake, baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika anakabiliwa na majeraha ya paja ambayo yatamuweka nje kwa siku kadhaa zijazo.

Taarifa hizo za kukosekana kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, zimepokelewa kwa huzuni na mashabiki wa klabu ya AC Milan ambao wameonyesha kumkubali tangu mwanzoni mwa msimu huu baada ya kusajiliwa akitokea Genoa kwa ada ya Euro million 20.

Yanga Wakubali Kumuachia Mkwasa
January Makamba: Bila Taifa Mshindi Ni Lofa