Mwanamke mmoja amesababisha mauti ya jirani yake kwa kumchoma kisu baada ya kuibuka mgogoro kati yao kuhusu chupa ya pombe huko nchini India.

Mwanamke huyo raia wa Tanzania na mkazi wa Dar es salaam, alikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya maafisa wa polisi kuukuta mwili wa marehemu nyumbani kwa mwanamke huyo ukiwa na majeraha.

“Tulipokea simu majira ya saa mbili na dakika kumi usiku kutoka kwa mwanamke mmoja raia wa Kenya akidai kwamba dadake ameuawa, tulikimbia katika eneo la mkasa na kumpeleka mwanamke huyo hospitalini ambapo daktari alisema kwwamba tayari alikuwa amefariki” alieleza kamishna wa polisi wa wilaya ya kusini Vijay Kumar.

Kulingana na na taarifa ya kamishna huyo wa Polisi, rekodi za mawasiliano ya simu na kanda za video za CCT zilitathminiwa ambapo mtuhumiwa ambaye alikuwa akiishi jirani na marehemu alikamatwa.

Alipohojiwa na polisi mtuhumiwa aliwaambia maafisa hao kwamba siku mbili zilizopita alikuwa amemtaka marehemu kumpatia pombe swala ambalo alikataa, ni wakati huo ambapo walianza kurushiana maneno kabla ya mshtakiwa kumchoma kisu marehemu.

kwamujibu wa gazeti la Nation la Kenya, mtuhumiwa na mpenzi wake walikuwa nyumbani kwao wakti mgogoro huo ukitokea lakini wawili hao walitoroka lakini walipatikana na kushirikishwa katika uchunguzi.

Ambapo mume wa mtuhumiwa amekiri kwamba mpenzi wake alikosana na marehemu kuhusu chupa ya pombe.

Hadi sasa ushahidi mwengine uliopatikana ni kisu pamoja na nguo ambazo mshukiwa alikuwa amevaa wakati wa kisa hicho zilizopatikana nyumbani kwake.

 

 

Capello: Real Madrid ilifanya makosa kumuuza Ronaldo
Fahamu mambo muhimu kuhusu hedhi kwa mwanamke

Comments

comments