Aliyekua katibu mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Amr Fahmy, ametangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho katia uchaguzi ujao ambao umepangwa kufanyika mwakani.

Fahmy aliyeingia madarakani kama katibu mkuu wa CAF kuanzia Novemba 2017 hadi Aprili 2019, ametangaza dhamira hiyo, huku akitambua wazi huenda akapata upinzani kutoka kwa Rais wa sasa Ahmad.

“Nitaanza kampeni zangu kwa kuzitembelea nchi za Sudan na Ethiopia mwezi Februari mwakani, nimepanga kuanza na nchi hizo kwa sababu zipo karibu na Misri na zilikua wanachama wa kwanza wa CAF,” alisema Fahmy alipohojiwa na BBC Sport.

“Babu yangu Mourad Fahmy alikua mmoja wa wajumbe walioiasisi CAF, pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa shirikisho hili, kama ilivyokua kwa baba yangu.”

“Wazee hawa wamelifanyia makubwa soka la Afrika, na ninaamini ni wakati wangu kuingia katika uongozi wa juu, ili kuendeleza dhamira ya kusaidia soka la Afrika.”

“Kampeni zangu zitaangilia sana weledi wa soka la Afrika, ili kuondokana na changamoto ikiwepo rushwa, ambayo ni tatizo kubwa katika makuzi ya mchezo huo barani kwetu.”

Babu yake Fahmy (Mourad) aliliongoza shirikisho la soka barani Afrika kama katibu mkuu kuanzia mwaka 1961-1982.

Baadae mwanawe Mustapha alirithi nafasi hiyo hadi mwaka 2010, kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho la soka duniani FIFA.

Lampard: Nitamtumia Abraham dhidi ya Aston Villa
Ethiopia yajichomoa CECAFA Senior Challenge Cup

Comments

comments