Mwanaume mmoja mkazi wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita, aliye julikana kwa jina la Selemani Mashauri (37), amemuua kwa kumyonga mkewe, Teddy Maro akimtuhumu kuwa kamwambukiza Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Baada ya kutekeleza mauaji hayo, Mashauri anadaiwa  kujiua na yeye pia kwa kujinyonga huku akiacha ujumbe unaoelezea sababu za vifo vyao ambavyo alivitekeleza yeye mwenyewe mjini Igunga ambako wana ndoa hao walienda kutembelea ndugu.

Kamanda wa polisi mkoani Tabora amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa yalitokea desemba 29,2018 mjini igunga.

Moja ya majirani wanyumba ambapo mauaji hayo yametokea ambaye hajataka kutajwa jinalake amesema “Baada ya kumuua mkewe Mashauri aliuficha mwili wake uvunguni mwa kitanda kabla nayeye hajachukua uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia mkanda wake wa suruali”.

Aidha ameongeza kuwa licha ya ujumbe ulioachwa na Mashauri kutajwa kuambukuzwa VVU, chanzo kingine cha mauaji hayo ambacho kilichochea kinatajwa kuwa ni maongezi ya simu aliyokuwa anayafanya marehemu Teddy,kwani hayakumfurahisha mumewe na alisikika akimtuhumu kuwa sio muaminifu.

Songea yakwama kukopesha Wanawake na Vijana
Nyani avamia na kushambulia wanakijiji

Comments

comments