Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans Boniface Ambani, raia wa Kenya amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao manne kwa moja  ilichokutana nacho klabu yake ya zamani kutoka kwa Simba SC.

Ambani amesema haikuwa rahisi kukubaliana na hali ya matokeo ya mchezo huo wa Nusu Fainali Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC) lakini ilimlazimu kuamini ni kweli klabu aliyowahi kuitumikia imepoteza mchezo.

Kutokana na hali hiyo Ambani ameutaka uongozi wa Young Africans kuboresha kikosi kwa sababu kimeonyesha bado hakina uwezo wa kupigania mataji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Ni matokeo ambayo hayajanifurahisha hata kidogo, kufungwa mabao manne dhidi ya Simba haileti picha nzuri kwa timu kubwa Kama Young Africans, lakini pia ni muamko kwa viongozi waangalie, na wajue kwamba hawana timu ambayo inaweza kupigania mataji katika ukanda huu”

“Kipindi cha usajili kinakuja, hakuna haja ya kuwa na wachezaji zaidi ya 30 ambao hawaisaidii timu afadhali kuwe na wachezaji 25 wanaoweza kusaidia timu halafu pesa ambazo wanawalipa wachezaji hao zaidi ya watano watafute wachezaji wa maana wa kuisaidia klabu.”

Picha: Wagombea CCM waliochukua fomu, Mtoto wa Lowassa akiwemo
Msimamo wa NEC nyongeza, punguzo ya majimbo 2020