Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamesonga mbele katika michuano ya kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Ihefu FC.

Bao la Ihefu FC lilikuwa la kujifunga baada mpira wa chini kumshinda mlinda lango Youthe Rostand kisha kumgonga beki Andrew Vicent na kutumbukia wavuni.

Pengine mazingira ya uwanja yalipelekea mpira huo kubadili mwelekeo kabla ya kumpoteza kipa Rostand.

Yanga walikosa nafasi kadhaa za wazi kupitia kwa washambuliaji wake Obrey Chirwa na Amissi Tambwe aliyekosa bao la wazi kwenye dakika ya kwanza ya mchezo.

Kipindi cha pili Yanga walitumia muda mwingi langoni mwa Ihefu lakini mlinda lango Andrew Kayuni alikuwa kikwazo kikubwa.

Yanga walisawazisha dakika za majeruhi kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Obrey Chirwa kwenye dakika za lala salama baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi.

Yanga wakaweza kusahihisha makosa yake kwenye mikwaju ya penati na kuibuka na ushindi wa penati 3-4

Kelvin Yondani, Hassani Kessy, Raphael Daudi na Gadiel Michael walifunga penati nne za Yanga huku Tshishimbi akikosa mkwaju wake.

Youthe Rostand alikuwa shujaa wa Yanga baada kuikoa timu yake kwenye mikwaju ya penati.

Vijana wa Ihefu FC walionyesha upinzani mkali kwa Yanga, wanastahili pongezi kwa upiganaji wao lakini uzoefu umeipa mafanikio Yanga siku ya leo

Vigogo wengine Azam FC wamesonga mbele kibabe baada ya kuichapa Shupavu FC ya mkoani Morogoro kwa mabao 5-0

Matokeo ya michezo iliyochezwa leo.

Tebas atamani kumrudisha Neymar Hispania
Video: Afrika kujitegemea kiuchumi, yaanza kuzalisha umeme wa kutosha