Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyakazi wake wa ndani aitwaye Salome Zakaria Machi 16, 2020, Mkami Shirima mwenye umri wa miaka (30), leo Machi 26, 2020, amefikishwa kwa mara ya pili katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kwa ajili ya kesi yake kutajwa.

Wakili wa serikali Abelaide Kasala ameema mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Amalia Mushi, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu mfawidhi Mushi amesema kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 8, 2020, itakapotajwa tena na mtuhumiwa kurudishwa rumande.

jinsi tukio lilivyotokea soma hapa Mfanyakazi auawa kwa tuhuma za kuiba elfu 50

Hata hivyo mtuhumiwa amesomewa pia kesi nyingine ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi ambayo ilitajwa kwa mara ya kwanza septemba 24, 2019.

Mgonjwa wa Corona aliyefariki kenya alikuwa na Kisukari
Kenya: Serikali yapiga marufuku uuzaji wa Chloroquine

Comments

comments