Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza, Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza mara baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo kustaafu.

Kabla ya uteuzi huo, nafasi ya Kamishna Jenerali ilikuwa inashikiliwa na Juma Alli Malewa ambaye mnamo Julai 6, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alimfukuza kikaoni kwa kuchelewa dakika moja yaani saa 5:01 badala ya saa 5:00, kinyume cha nidhamu ya jeshi.

Aidha uteuzi huo umefanyika mapema leo, Julai 13, 2018.

Mlipuko wa tenki la kemikali wajeruhi, Jeshi lanena
Balozi wa China amkabidhi Makonda majengo ya ofisi za walimu

Comments

comments