Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Bi Paulina Mlenga (35), kwa tuhuma ya mume wake, Soud Mdoka  aliyehusika katika mauaji ya jirani yao aliyefahamika kwa jina la Mohammed Hamimu aliyeuliwa kwa kupigwa na bomba la chuma kichwani.

Mauaji hayo yalitokea Februari 12 mwaka huu majira ya Saa 3 usiku katika mtaa wa pachannenLizboni wakati wa ugomvi wa wanandoa hao Soud Mdoka na Paulina Mlenga.

Taarifa hizo zimethibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma, Gemin Mushy aliyethibitisha kutokea kwa tukio hilo mkoani kwake.

Ambapo marehemu ambaye alikuwa jirani  ya wanandoa hao aliamua kuingilia na kutaka kusuluhisha ugomvi wa wanandoa hao ndipo Mdoka alipoamua kuchukua bomba la chuma na kumpiga nalo kichwani kwenye utosi na kumsababishia kifo papo hapo.

Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo mtuhumiwa aliyehusika na mauaji hayo aliamua kukimbia kusikojulikana.

Juhudi za kumtafuta bado zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi, huku mke wa mtuhumiwa huyo akiwa mabroni wakati upelelezi ukiwa unaendelea.

 

Manispaa ya Ilala yatoa mkopo wa shil. mil. 153 kwa vikundi
Lugola aagiza mkurugenzi wa kampuni Arusha asukumwe ndani

Comments

comments