Mwanamke mmoja nchini Somalia amepigwa mawe mpaka kufa baada ya mahakama inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, Al-Shabaab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.

Shukri Abdullahi Warsame alituhumiwa kuolewa mara 11 bila kutalikiwa na waume zake waliopita hivyo kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo alihukumiwa kuuawa.

Aidha, sehemu ya kiwiliwili chake kilifukiwa ardhini kichwa kikiachwa juu kisha akapigwa mawe na wanamgambo mjini Sablale mpaka umauti.

Hata hivyo, mwaka 2014,wapiganaji wa Al-Shabaab walimpiga mwanamke mmoja kwa mawe baada ya kumtuhumu kuolewa na wanaume wanne kwa siri katika wilaya ya Barawe nchini humo.

Sugu, Masonga waachiwa huru
Video: Serikali yacharuka sakata la mafuta ya kula, Dawa kinga ya Ukimwi yazinduliwa