Muigizaji wa series maarufu ya ‘Power’, Omari Hardwick huenda akawa anauguza maumivu ya madonda ya kisaikolojia baada ya kushambuliwa na mamilioni ya mashabiki wa Beyonce ‘Beyhive’ wanaofananisha mashambulizi yao na nyuki, waliokerwa na kitendo cha kidume huyo kumpiga mabusu Malkia Bey mbele ya mumewe, Jay Z.

Omari Hardwick alikutana na Beyonce na Jigga kwenye tuzo za NAACP 2019, zilizofanyika Aprili Mosi, ambapo aliingia kuwasalimia. Alianza na Jay Z akapiga naye picha. Akamfuata pia Beyonce na kumkumbatia kisha akampiga busu la kwanza, lakini wakati mwimbaji huyo akidhani yamekwisha ki-salamu alipigwa busu lingine kwenye kona ya mdomo wake hali iliomfanya aonekane amekosa amani ghafla.

Jay Z hakuona mali yake ilivyofanyiwa, na jamaa alivyo na wivu, angeona sijui ingekuwaje. Lakini kwa bahati nzuri, ana walinzi na kikosi kazi cha makomandoo mtandaoni wanaojiita ‘nyuki wa Beyonce’, mashabiki wanaofahamika kwa jina la kizungu kama ‘Beyhive’.

Wengi wameonesha kuumizwa na busu la pili la karibu na mdomo, wengine wamejieleza kama wanawake wakidai kuwa wanapinga tabia ya wanaume kutumia fursa ya matamasha kuwashika au kuwabusu kwa namna ambayo hawakutarajia.

“Busu la pili hakuwa na ulazima na halikubaliki. Usirudie tena,” shabiki mmoja alitweet. “Sisi wanawake hushikwa, kubusiwa, na kufanyiwa vitendo vingi kwenye matukio kama haya ya tuzo. HATUPENDI. Ni muda wa kupinga na kukataa matendo haya,” alitweet mwingine.

Hata hivyo, tweet zilikuwa na afadhali, mashabiki wa Beyonce ‘Beyhive’ walimfungia kibwebwe Omari Hardwick kwenye Instagram. Kwenye kila post aliyoweka walijaa kama nyuki wakiweka picha ya vinyuki kabla ya kumshambulia kwa maneno makali na ya kuudhi.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 5, 2019
Lema azungumza baada ya kuadhibiwa bungeni, awapa ujumbe wabunge

Comments

comments