Mahakama ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imemhukumu Shabo Marando (47) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka bibi mwenye miaka 60.

Hakimu Mfawidhi Ester Malick, alitoa hukumu hiyo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliokuwa na mashahidi wanne.

Hakimu Malick akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 87 ya mwaka 2019, alichambua ushahidi wa shahidi watatu, Dkt. Judith Kiwango wa hospitali ya wilaya ambaye alimfanyia uchunguzi bibi huyo, aliyesema alimkuta na michubuko sehemu za siri pamoja na manii.

shahidi namba mbili Sama Luheka (34), mkazi wa kijiji cha Nange alisema Julai 9 mwaka huu huko Igokelo baada ya kusikia kelele katika vichaka alienda katika eneo hilo na kumkuta mtuhumiwa akimbaka bibi huyo.

Sumaye ajiondoa rasmi Chadema, amtumia ujumbe Mbowe ‘nimelazimishwa’

kwa upande wa bibi huyo ambaye alifanyiwa unyama, kwenye ushahidi wake alidai kuwa anamfahamu mtuhumiwa kuwa ni mkazi wa kijijini kwake.

Na kudai kuwa siku ya tukio alikuwa shambani akikusanya kuni, mtuhumiwa alifika na kusalimiana, mara akamkamata kwa nguvu, kumvuta kichakani kisha akambaka.

Katika utetezi wake mtuhumiwa huyo alidai kuwa mlalamikaji ni shemeji yake, alimpa eneo la kulima na siku ya tukio alikamatwa na wananchi baada ya kuwa amechota maji ya kumwagilia nyanyazake kwa madai kwamba dimbwi alilochota maji lilisha zuiwa na kwamba si kweli kuwa alimbaka shemeji yake.

Awali mwendesha mashtaka wa Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Juma kiparo akisoma shtaka lake alidai Julai 9 mwaka huu katika kitongoji cha Igokelo, mtuhumiwa huku akifahamu kuwa ni kosa alimbaka bibi huyo na kumsababishia maumivu makali.

Kashfa ya kudanganya umri yamng'oa Mwenyekiti UVCCM Mtwara
Sumaye ajiondoa rasmi Chadema, amtumia ujumbe Mbowe ‘nimelazimishwa’

Comments

comments