Babu mwenye umri wa miaka 100 aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la mauaji nchini Nigeria ameachiwa huru kwa msamaha wa Serikali.

Celestine Egbunuche ameachiwa wiki hii akiwa ametumikia miaka 18 jela baada ya kukutwa na hatia ya kupanga mauaji.

Baada ya kuachiwa huru, alikutana na familia yake nje ya gereza la Enugu ambalo lina ulinzi mkali zaidi. Mwanaye, Chisom Celestine alieleza jinsi alivyofurahi kumuona tena baba yake uraiani.

“Nilifurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa siku hii. Mimi ni mtu mwenye furaha zaidi duniani sasa hivi,” alisema.

Egbunuche ambaye hivi sasa anasumbuliwa na magonjwa kama kisukari na matatizo ya kuona, amewekwa chini ya uangalizi wa kimatibabu hospitalini.

Hata hivyo, mwanaye amesema kuwa hana uwezo wa kifedha wa kumsaidia baba yake kupata matibabu.

Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imeendelea kufanya kampeni kutafuta namna ya kumsaidia.

Rais Magufuli atoa siku 30 kwa kampuni zinazokwepa kulipa kodi
Neymar ahojiwa polisi kuhusu tuhuma za ubakaji, azungumza na mashabiki