Fatuma Selemani Chikawe, mkazi wa kigamboni amemuomba radhi aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kufuatia kashfa aliyomzushia akidai kuwa ni baba yake aliyemtelekeza.

Mwanamke huyo ameomba radhi na kujutia alichokifanya kwani hakutegemea kama ingekuwa hivyo ambavyo watu wameichukulia kisiasa, amedai kuwa ni siku nyingi amekuwa akimtafuta Lowassa ili amsaidie ila jitihada hizo ziligonga mwamba ndipo alipoamua kutumia njia hiyo.

”Nilikuwa naomba radhi kwa kilichotokea mitandaoni ambapo nimemdhalilisha mzee ambaye ni Edward Lowassa mtandaoni, lakini sikutegemea kama ingekua vile, nilienda vile kama kuomba msaada anisaidie sababu miaka mingi namtafuta mzee, lakini kilichotokea hata mimi nafsi yangu inaniuma na sikutegemea kama ingekuwa vile sina amani, kwenye familia yangu, mtaani najuta sababu najua huyo mzee nimemkwaza kwa kiasi fulani sababu yeye ana familia yake ana watoto wake, sijajua wamelipokea vipi, pia hilo linaniuma na mzee kama yule kumuweka kwenye mitandao roho inaniuma kwahiyo naomba aniwie radhi anisamehe kwa kilichotokea, mambo yametumika kisiasa, nashambuliwa na maneno sina amani na maisha yangu na familia yangu”. amesema Fatma.

Kufuatia zoezi linaloendelea jijini Dar es salaam, ambapo Mkuu wa Mkoa wa huo, Paul Makonda ameamua kuwasaidia kisheria wanawake waliozalishwa na kutelekezwa, Fatma alijitokeza akidai kuwa baba yake ni Edward Lowassa na ameanza kumtafuta tangu akiwa darasa la sita bila mafanikio.

Hata hivyo Lowassa alihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kufuatia kashfa hiyo alikanusha kuhusika na mtoto huyo na alidai kuwa  kupima DNA ”vina saba” ni upuuzi.

 

RC Makonda asitisha wanafunzi kwenda shule, TMA yatoa utabiri
Pep Guardiola afikisha taji la 24, Man City 7