Mwanume ambaye alichomwa visu kichwani na mgongoni alipokuwa anamsaidia mwanamke aliyekuwa anabakwa, nchini Afrika kusini, amependekezwa kuwania tuzo ya mwanaume bora wa mwaka, nchini humo.

Radius Masukume (49), alikuwa anatembea katika eneo la wazi Oktoba 10 mwaka huu na akasikia sauti ya mwanamke analia kwa kuomba msaada, alipoelekea eneo la tukio aliwakuta vijana wadogo wawili wanambaka mwanamke wa miaka 45.

Alipojaribu kumuokoa mama huyo, alichomwa na visu kichwani na mgongoni na kumsababishia maumivu makali yaliyomfanya akimbie kuomba msaada zaidi.

Alipokuwa barabarani alibahatika kuwakuta maafisa polisi waliokuwa kwenye doria na kutumia mwanya huo kuripoti tukio.

Tuzo hizo za mwanume bora wa mwaka hutolewa kwa kutambua mchango chanya wa mwanaume katika jamii inayomzunguka, mwaka huu itatolewa mwezi Novemba.

Mwenyekiti wa uandaaji wa tuzo hizo Bongani Ngomane, amesema kuwa Masukume anastahili kupata tuzo hizo na sio kwaajili ya watu wa rasi ya tumaini jema pekee bali kwa nchi nzima.

Hata hivyo tayari kampeni ya kuchangia fedha kwaajili ya kumpa Masukume imefanyika ili ibaki alama juu ya usujaa wake alio uonesha.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 28, 2019
Mwanafunzi atoa mimba na kutupa chooni wazazi ,viongozi wa dini wafunguka