Mfaransa mweusi, mwenye asili ya Mauritania, ambaye alitukanwa na kubaguliwa kwa rangi yake na mashabiki wa timu ya Chelsea kwenye kituo cha treni mjini Paris mwezi Februari, amesemaa anataka waliomtusi wapandishwe kizimbani kwenye mahakama ya Ufaransa.

Mkanda wa video ulioonyesha kundi la mashabiki wakimzuia Bwana Souleymane Sylla kupanda treni huku wakipiga mayowe wakisema “sisi ni wabaguzi wa rangi na hivyo ndivyo tunavyopenda”.

Katika mahojiano na BBC, Souleymane Sylla alisema: “nataka fidia kwangu na kwa familia yangu”.

“Wanangu wamefadhaishwa- mimi pia lakini ni athari kwa watoto wangu ndio inaumiza zaidi. ”Bado sijaridhika. Nataka waletwe kutoka Uingereza wapelekwe mbele ya sheria katika nchi yangu.”

Mashabiki hao wanne walipigwa marufuku kuhudhuria mechi za soka kwa miaka mitanokatika kesi iliyoamriwa nchini Uingereza Jumatano wiki hii.
Watu hao hawajawahi kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu nchini uingereza kuhusiana na tukio hilo.

Hamad Rashid Aiunganisha CUF na CCM
Van Persie Aikabidhi Familia Yake Fenerbahce