Diamond Platinumz leo amefanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amefunguka kuhusu baadhi ya vyombo vya habari ambavyo havifanyi kazi zake wala za wasanii wake, amesema kuwa yeye hashindani na mtu.

Kufuatia hatua hiyo iliyochukuliwa na vyombo hivyo amesema iliwapa nguvu timu nzima ya Wasafi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuwasaidia wasanii wengine ambao wanakutana na changamoto hiyo.

Amesema hawezi kulaumu media yeyote ambayo haipigi kazi zake kwani mpaka sasa kuna zaidi ya media nne ambazo hazipigi kazi zake.

Na kusisitiza kuwa Wasafi Media imeanzishwa si kwa ajili ya kushindana na chombo chochote kwani kila chombo kina nafasi yake na kitaendelea kuwepo na kila chombo kina mtazamo wake.

”Hatuna nia ya kugombana na chombo chochote, kuonesha sisi bora kuliko chombo chochote, tunaonesha tulichojaliwa na mwenyezi Mungu kidogo chetu hicho hicho.” amesema Diamond

Aidha amewaomba watu wasiogope kuleta kazi zao ili wapewe sapoti kwani kupitia Wasafi Media wasanii wengi sasa nyimbo zao zimeanza kupigwa katika vyombo vingine vya habari.

Merkel, Macron wateta kuhusu mzozo wa Umoja wa Ulaya
Majaliwa atoa agizo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya