Saa chache baada ya Diamond Platinumz kueleza kuwa wamemualika Ali Kiba kwenye ‘Wasafi Festival’ itakayofanyika Novemba jijini Dar es Salaam, mkali huyo wa ‘Seduce Me’ amejibu kwa lugha kali.

Ali Kiba ametumia akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni 4.5 akieleza kuwa anaweza kumuweka uchi Diamond kwa madai kuwa amemfanyia mambo yasiyo ya heri nyuma ya pazia, akitoa mfano wa mtu aliyemuibia na baadaye anajidai anamsaidia kutafuta alichoibiwa.

“Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta (UNIKOME).  Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz. #KingKiba” ,” ameandika Ali Kiba.

Huu ni ujumbe mkali zaidi kuwahi kutokea kwa Ali Kiba kwenda kwa Diamond hadharani. Mara ya mwisho wawili hao kujibishana mitandaoni kufuatia moto uliowashwa na cheche za wimbo wa ‘Fresh’, alioufanya Diamond ikiwa ni Remix ya wimbo wa Fid Q.

Kwenye wimbo huo, Diamond alimkwaruza Ali Kiba, naye akajibu kwenye Instagram na Twitter.

Vita hiyo ya maneno ilizimika kwa muda baada ya Ommy Dimpoz kuhusika na akatoa maneno makali zaidi yaliyomgusa Mama yake Diamond. Hatua hiyo ilikosolewa na wengi na kulaani kauli iliyolewa na mwanafamilia huyo wa Rockstar Africa.

Hii ni mara ya pili kwa Alikiba kukataa kutumbuiza kwenye tamasha hilo la Wasafi Festival, alifanya hivyo pia mwaka jana ambapo alisema yupo tayari kutoa udhamini kupitia kinywaji chake cha Mo Faya badala ya kufanya show.
Hii ni ‘post’ya Ali Kiba:

Halmashauri na taasisi za kifedha zatakiwa kukopesha vijana
Sheria ya mfumo wa nidhamu kazini yapikwa

Comments

comments